Waziri wa Afya katika kaunti ya Nakuru Roselyn Mungai amesema kuwa serikali ya kaunti imeweka mipangilio kabambe kuhakikisha kuwa huduma za afya katika hospitali ya Elburgon zinaimarishwa.Akizungumza wakati wa ziara yake katika hospitali hii alipofanya mkutano pamoja na bodi ya usimamizi, Mungai alisema kuwa mipango hii inayonuia kuanza kutekelezwa baada ya mwezi mmoja italeta ongezeko la wateja wanaohudumiwa mjini Elburgon na hata maeneo jirani kwa mara mbili zaidi.Ili kufanikisha juhudi hii, waziri alisema kuwa tayari ununuzi wa vifaa muhimu vya matibabu unaendelea na vitawezesha pia kuboresha miundombinu muhimu hospitalini kama vile katika chumba cha kujifungulia cha akina mama, chumba cha upasuaji, picha baadhi ya maeneo mengine pia.Aidha, Mungai alisalia na imani kuwa ikiwa hatua hizi zitatekelezwa, basi bila shaka changamoto nyingi zitaweza kushughulikiwa akiwaomba wafanyikazi mahala pale kuendelea kuyasikiliza matakwa ya wakaazi katika utoaji huduma bora ya afya ili wawe katika mstari wa mbele k uwahudumia vilivyo.Kwa muda, hospitali hii imekuwa na uwezo wa kushughulikia wagonjwa 3,000 kwa siku.Source: Kenya News Agency
Recent Posts
EAC Unveils Strategy to Harness Aquatic Resources
November 22, 2025
Government Emphasizes Research-Focused Funding for Universities
November 22, 2025
Bishop Kimengich Calls for Peace in Volatile Kerio
November 22, 2025
Six Lives Lost in Tragic Accident on Ngoluni-Tawa Road
November 22, 2025
CS Mugaa Inspects Sh1B Irrigation Canal Project in Mwea
November 22, 2025